Eneo Huru la Biashara la Bara la Afrika (AfCFTA) - Utafiti kwa “Wafanyibiashara Wanawake”

Eneo Huru la Biashara la Bara la Afrika (AfCFTA) – eneo kubwa zaidi la biashara-huru ulimwenguni – ilianza kufanya biashara mnamo tarehe 1 Januari 2021 na kutengeneza soko la watu bilioni 1.2. Katika mkutano wa dharura wa viongozi wa mataifa na serikali za Muungano wa Afrika, uliofanyika Desemba 2020, uongozi wa AfCFTA ulielekezwa kuanza kazi ya kuandika itifaki ya Wanawake katika Biashara.

UN Women, kwa ushirikiano na uongozi wa AfCFTA na UNDP, inafanya utafiti ili kuelewa changamoto na nafasi ambazo wanawake na biashara zinazoongozwa na wanawake zinakumbana nazo maadamu kuanzishwa kwa Eneo Huru la Biashara la Bara la Afrika. Ufafiti huu unalenga (i) kubainisha vizuizi na vikwazo vinavyowazuia wanawake kushiriki katika biashara (ii) kutambua nafasi zilizoko na madhara ya AfCFTA kwa wanawake na biashara zinazoongozwa na wanawake. Matokeo ya utafiti huu yatatumika katika mikakati ya kuunda itifaki ya Wanawake katika Biashara ya AfCFTA.

Majibu yote yatatunzwa kisiri na wenye data hizo hawatajulikana iwapo zitatumika nje ya UN Women.

Utafiti huu utachukuwa kadri ya dakika 15 kukamilisha.

show filters hide filters